• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Guardiola kuagana na Man-City 2023 akimezea ukocha wa timu ya taifa

Guardiola kuagana na Man-City 2023 akimezea ukocha wa timu ya taifa

Na MASHIRIKA

KOCHA Pep Guardiola aliyetia saini mkataba mpya ugani Etihad mnamo Novemba 2020, ametangaza kwamba ataagana rasmi na Manchester City mwishoni mwa msimu wa 2022-23.

Kufikia wakati huo, Guardiola, 50, atakuwa amewajibikia Man-City kwa kipindi cha miaka saba.

Kwa mujibu wa mkufunzi huyo raia wa Uhispania, mipango yake baada ya msimu huo wa 2022-23 ni kuwa kocha wa timu ya taifa.

“Nitapumzika kidogo baada ya miaka saba kambini mwa Man-City. Muda huo wa mapumziko utanipa fursa ya kujifunza mengi kutoka kwa makocha wa timu mbalimbali za taifa ili nami mifuate mkondo huo,” akasema kwa kusisitiza kwamba maazimio yake ni kuongoza timu zitakazomvunia mataji ya Euro, Copa America na Kombe la Dunia.

Baada ya kuagana na Barcelona mnamo 2011-12, Guardiola alipumzika kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuajiriwa na Bayern Munich ya Ujerumani kujaza nafasi ya Jupp Heynckes mnamo Juni 2023.

Japo aliongoza Bayern kunyanyua mataji matatu ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na makombe mawili ya German Cups, alishindwa kutwalia kikosi hicho taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Ufalme wa UEFA ni taji ambalo limezidi kuteleza mbele ya Guardiola huku waajiri wake Man-City wakizidiwa maarifa na Chelsea kwa kichapo cha 1-0 kwenye fainali ya kipute hicho mnamo 2020-21 jijini Porto, Ureno.

Baada ya kuanza vibaya kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2021-22 kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Tottenham Hotspur, Man-City walijinyanyua katika mechi ya pili na kuwapepeta Norwich City 5-0 mnamo Agosti 21, 2021.

Mabingwa hao watetezi wa EPL watavaana na Arsenal mnamo Agosti 29, 2021 ugani Etihad katika mchuano wa tatu wa EPL muhula huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Siraj: Nitasalia Harambee Stars

FAO yajikakamua kuchangisha fedha kuokoa kaunti 23...