• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Umuhimu wa madini ya zinki mwilini

Umuhimu wa madini ya zinki mwilini

Na MARGARET MAINA

[email protected]

ILI mwili wa mwanadamu uweze kukaa na kunawiri vizuri, ni lazima upate virutubisho vinavyoitwa madini.

Tutazame madini yajulikanayo kwa kimombo kama madini ya zinc (zinki).

Inakadiriwa kuwa mwili wa mwanadamu una hadi gramu mbili (2) za zinki, ambapo asilimia 60 hupatikana kwenye misuli na thelathini kwenye mifupa, ingawa hupatikana mwili mzima.

Zinc inatekeleza majukumu mbali mbali mwilini ambapo imeonyesha kuimarisha kinga ya mwili, kuimarika kwa mfumo wa fahamu, huboresha sukari mwilini, hupambana na mafua, huimarisha uponaji wa vidonda, husaidia kukabili matatizo ya akili, matatizo ya kupoteza hamu na ladha ya chakula, matatizo ya sikio, na kadhalika.

Vyakula vyenye madini ya zinc kwa wingi

  • nyama
  • mayai
  • samaki wa baharini
  • njugu na jamii nyingine za karanga
  • nafaka
  • uyoga
  • mbegu za maboga
  • jamii ya maharage ya kijani

Dalili za ukosefu wa madini ya zinc mwilini

  • kupoteza hamu na ladha ya chakula
  • ukuaji wa kusuasua kwa mtoto
  • upungufu wa kinga ya mwili
  • vidonda kuchelewa kupona
  • kupoteza uwezo wa kuona
  • mabadiliko ya tabia hasa uchovu wa mara kwa mara
  • mtoto kuzaliwa na vilema au ulemavu
  • mtoto kuzaliwa na uzani mdogo.

You can share this post!

JAMVI: Mradi watia doa azma ya Shahbal kuwania ugavana

Arsenal kutamatisha mkataba wa Willian anayetaka kurejea...