• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 11:55 AM
Crystal Palace yapiga Spurs breki kali katika EPL

Crystal Palace yapiga Spurs breki kali katika EPL

Na MASHIRIKA

ODSONNE Edouard alifunga mabao mawili katika mchuano wake wa kwanza ndani ya jezi ya Crystal Palace na kusaidia kikosi hicho kusajili ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.

Matokeo hayo yalikomesha rekodi nzuri ya kutoshindwa kwa Spurs katika mechi nne mfululizo katika EPL hadi kufikia sasa muhula huu.

Wilfried Zaha alifungulia Palace ukurasa wa mabao kupitia penalti iliyotokana na hatua ya beki Ben Davies kunawa mpira ndani ya kijisanduku.

Edouard aliyeingia ugani katika kipindi cha pili aliongeza mabao mengine mawili ya Palace ambao kwa sasa wananolewa na kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Patrick Vieira.

Edouard ambaye ni fowadi raia wa Ufaransa, alisajiliwa na Palace muhula huu kutoka Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland. Mabao yake dhidi ya Spurs yalikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Zaha pamoja na Conor Gallagher.

Ushindi huo ulipaisha Palace hadi nafasi ya 11 kwa alama tano.

Spurs walikamilisha mchuano huo na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya Japhet Tanganga kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 58.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Wakfu wa Jungle Foundation watoa mafunzo ya huduma ya...

Ronaldo afunga mabao mawili Man-U ikicheza dhidi ya...