• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
Vyakula vinavyoimarisha afya ya macho

Vyakula vinavyoimarisha afya ya macho

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KUIMARISHA nuru ya macho yako kwa kiasi kikubwa kunaanza na chakula.

Lishe ya vyakula vya asili hukupa virutubisho unavyohitaji ili afya ya macho iimarike na vyenyewe (virutubisho) ni kama vile asidi ya mafuta ya omega-3, zinki na vitamini C na E.

Vyakula vinavyohitajika kwa macho yenye afya

Macula yako iliyoko katikati ya jicho la jicho, ndicho kitovu cha kutuwezesha kuona vizuri na hasa rangi. Vyakula vyenye oxidants husaidia kulinda seli zetu dhidi ya sumu kali kali.

Zoea kula vyakula vyenye carotenoids, rangi ambazo hutokea kawaida katika mimea.

Vyakula bora kwa afya nzuri ya macho

Kuna baadhi ya vyakula bora ambavyo unaweza kula kwa ajili ya afya ya macho yako

Pilipili nyekundu

Pilipili nyekundu. Picha/ Margaret Maina

Kumbuka, mmea wowote au mboga ambayo ina rangi ya manjano au rangi ya machungwa ina hizi carotenoids. Pilipili nyekundu pia husaidia macho kupata vitamini C.

Mayai

Mayai pia yana viwango vya juu vya lutein na zeaxanthin. Chembechembe hizi kawaida huingizwa kwa urahisi na mwili zikiwa kwenye mayai kuliko kutoka kwa mboga kwa sababu ya mafuta yaliyomo.

Samaki

Samaki huwa na asidi muhimu ya mafuta ambayo mwili wako na macho yako hutegemea. Ikiwa unakosa asidi ya mafuta ya omega-3, kama ile inayopatikana kwenye samaki wa mafuta, unaweza kujikuta ukiwa na macho makavu.

Karanga na mbegu

Vitamini E ambayo hupatikana kwa wingi kwenye karanga na mbegu husaidia kulinda seli zilizo machoni mwetu. Mbegu za alizeti au mlozi zitakupa zaidi ya thuluthi moja ya aina hii ya vitamini kila siku.

Matunda ya machungwa

Vitamini C inapatikana kwa wingi kutoka kwa machungwa na matunda ya zabibu. Aina hii ya vitamini husaidia kuimarisha kinga.

Nafaka nzima

Vyakula hivi vinaweza kusaidia macho yako. Hiyo inamaanisha vyakula vya wanga kutokna na ngano iliyosafishwa kama mkate mweupe achana navyo. Unatakikana uanze kula quinoa, wali wa kahawia na mkate wa ngano ya kahawia yaani brown bread. Vyakula hivi pia vinakupa zinki na vitamini E, ambayo husaidia kukuza afya ya macho kwa ujumla.

Karoti

Labda umesikia juu ya karoti na matunda na mboga nyingine zenye rangi ya machungwa kwamba husaidia kuimarisha afya ya macho. Sababu kuu ni kwamba huwa na Beta-carotene, aina ya vitamini A ambayo huvipa vyakula hivi rangi ya machungwa na ni muhimu kwa macho kwa sababu inasaidia retina na sehemu nyingine za jicho kufanya kazi vizuri.

Viazi vitamu

Viazi vitamu vina virutubisho sawa na karoti ambavyo vinaimarisha afya ya macho.

You can share this post!

Wasichana 6 watimuliwa shuleni kwa mihadarati

ULIMBWENDE: Tengeneza maski ya nywele kwa kutumia...