• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 10:55 AM
‘Unywaji wa kahawa una madhara pia’

‘Unywaji wa kahawa una madhara pia’

Na MARGARET MAINA

[email protected]

UNYWAJI wa kahawa umezoeleka na ukawa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Kemikali iliyopo ndani ya kahawa kwa kitaalamu inaitwa caffeine.

Kahawa inakuwa kama unga mweusi mchungu sana lakini hupelekwa viwandani na kubadilishwa na kuongeza vionjo.

Ukinywa kawaha baada ya dakika chache huingia kwenye damu na kusafiri mpaka kwenye ubongo.

Husababisha mtu kutoka kwenye utulivu na kumfanya achangamke.

Kahawa huzuia kemikali moja kitaalamu kwa jina la adenosine. Kwa hali ya kawaida adonosine huzuia kemikali ya uchangamfu kwa jina la acetycholine.

Kahawa pia humwaga homoni za adrenaline kwenye damu Homoni hizi huwa zinatengenezwa mtu akiwa na wasiwasi, uoga au hasira.

Sigara inaongeza kasi ya kazi ya kahawa mwilini hivyo wavuta sigara wakinywa kahawa inawaingia haraka kuliko watu ambao sio wavutaji.

Unywaji wa kahawa huleta faida za muda tu ambazo ni kama kuondoa usingizi na kukufanya usome au ufanye kazi kwa muda mrefu, huondoa uchovu na uvivu unapoinywa, ni nzuri kwa wagonjwa wa pumu kwani hupanua mirija ya hewa.

Watu wengine huweza kuondoa maumivu ya kichwa kwa kunywa kawaha, kimsingi dawa nyingi za kutuliza maumivu zina kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa.

Pamoja na faida zote hizo, kahawa ina madhara ambayo ni hatari kwenye mwili wa binadamu kama ifuatavyo.

Huongeza sukari mwilini

Kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa huongeza sukari mwilini kwa kuongeza kiwango cha adrenaline. Hii ni hatari sana kwa mgonjwa mwenye kisukari tayari.

Huongeza kukojoa

Kahawa hufanya mtu kukojoa mara kwa mara kitaalamu kama diuresis. Hali hii humletea mtu usumbufu mkubwa wakati wa kulala au wakati wa kazi.

Hupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula

Kemikali ya caffeine hufunika eneo la tumbo kwa kuweka kitu kama koti na kuzuia mmeng’enyo mzuri wa chakula. Magonjwa mbalimbali ya tumbo kama colitis huongezwa zaidi na kahawa.

Kukosekana kwa vitamini B

Caffeine hupotea pale kahawa inapotumika kwa wingi sana na hupunguza vitamini B ambayo ni muhimu sana kwenye kuvunja wanga na kuupa mwili nguvu.

Huleta madhara kwenye moyo

Kemikali ya caffeine husababisha moyo kupiga bila mpangilio maalumu. Hali hii inaweza kusababisha mshtuko wa moyo hasa kwa wagonjwa wa moyo.

Kukosa usingizi

Kahawa huharibu ubora wa usingizi. Mtu aliyekunywa kahawa anaweza kulala kwa kuhangaika sana huku akiamka mara kwa mara katikati ya usingizi. Mara nyingi wanafunzi wanaotaka kusoma muda mrefu usiku hunywa kawawa.

Humaliza nguvu za mwili

Ukinywa kahawa, unaufanya mwili ushindwe kupumzika kipindi unafanya kazi hivyo unakuwa una nguvu sana mwanzoni, baadaye kahawa ikiisha mwilini unajikuta na uchovu mkali sana.

Kuchosha figo na maini

Kemikali ya caffeine inafanyisha viungo hivi vya mwili kazi kupindukia. Baadaye viungo hivi huchoka sana na kupoteza ufanisi, Hii ndiyo sababu wagonjwa wa ini na figo hushauriwa kutotumia kahawa.

Chai ya kijani maarufu kama green tea ni nzuri sana kwa mwili wa binadamu kwa sababu hupunguza presha ya damu, huipa nguvu mishipa ya damu, hutibu magonjwa yasababishwayo na bacteria na kuzuia damu kuganda.

You can share this post!

ULIMBWENDE: Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi...

Wario na Soi watozwa faini ya Sh109Milioni ama kifungo cha...