• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Mashabiki watiwa nguvuni baada ya vurugu kuzuka wakati wa mechi ya Europa League katikati ya Leicester City na Napoli

Mashabiki watiwa nguvuni baada ya vurugu kuzuka wakati wa mechi ya Europa League katikati ya Leicester City na Napoli

Na MASHIRIKA

IDADI kubwa ya mashabiki walitiwa nguvuni baada ya vurugu kuzuka uwanjani kabla ya mechi ya Europa League iliyokutanisha Leicester City na Napoli mnamo Septemba 18, 2021.

Kwa mujibu wa polisi, mashabiki wanane wa Napoli na mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 27 kutoka Leicester walizuiliwa na maafisa wa usalama baada ya purukushani kuzuka hatua chache kutoka uwanja wa King Power.

Mwanamume mwingine mmoja mwenye umri wa miaka 39 kutoka Italia pia alizuiliwa kwa madai kwamba alimtukana dereva wa teksi.Maafisa wa usalama wa Leicestershire walisema “wamekabiliana naye kwa njia iliyoafikiwa na jamii”.

Mwanamume mwingine mwenye umri wa miaka 36 kutoka Anstey alihojiwa na polisi kwa kosa la ubaguzi wa rangi kabla ya kuachiliwa bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Maafisa wa usalama kutoka Leicestershire walisema mashabiki kutoka klabu zote mbili walirushiana vifaa uwanjani baada ya mechi hiyo iliyokamilika kwa sare ya 2-2 baada ya Napoli kutoka chini kwa mabao mawili na kusawazisha mambo.

Mashabiki wa Napoli walizuiliwa uwanjani kwa muda baada ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa. Mashabiki wanane wa Napoli na mwanamume wa Leicester wangali kizuizini wakihojiwa na polisi.

  • Tags

You can share this post!

Suluhu aashiria kugombea kiti cha urais mwaka 2025

Babake Ake wa Man-City afariki dunia saa chache baada ya...