• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Babake Ake wa Man-City afariki dunia saa chache baada ya beki huyo kufunga bao la kwanza la UEFA

Babake Ake wa Man-City afariki dunia saa chache baada ya beki huyo kufunga bao la kwanza la UEFA

Na MASHIRIKA

BEKI Nathan Ake wa Manchester City amefichua kwamba babake mzazi aliaga dunia dakika chache baada ya yeye kufunga bao lake la kwanza la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Ake, 26, aliwafungulia Man-City ukurasa wa mabao katika dakika ya 16 katika ushindi wa 6-3 uliosajiliwa na miamba hao wa soka ya Uingereza dhidi ya RB Leipzig ugani Etihad.

Kupitia ujumbe alioupakia kwenye mtandao wa kijamii, Ake alisema babake mzazi, Moise, alifariki pindi alipotikisa nyavu za Leipzig.“Najua mara zote uko nami. Utakuwa moyoni mwangu daima na bao hili nililolifunga ni kwa ajili yako,” akaandika kwenye Instagram.

Ake aliyeanza kucheza soka ya kulipwa akiwa Chelsea, amewajibikia Man-City mara 16 tangu atue ugani Etihad kutoka Bournemouth kwa Sh5.6 bilioni mnamo 2020. Kufikia sasa, anajivunia kuchezea timu ya taifa ya Uholanzi mara 22 tangu awajibishwe kwa mara ya kwanza mnamo 2017.

  • Tags

You can share this post!

Mashabiki watiwa nguvuni baada ya vurugu kuzuka wakati wa...

Shujaa yaendea Uhispania kulipiza kisasi raga ya Vancouver...