• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:20 AM
Watford warefusha mkia wa Norwich City kwenye jedwali la EPL

Watford warefusha mkia wa Norwich City kwenye jedwali la EPL

Na MASHIRIKA

ISMAILA Sarr alifunga mabao mawili na kuwezesha Watford kupiga Norwich City 3-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Matokeo hayo yalisaza Norwich ambao pia walipandishwa ngazi kushiriki EPL msimu huu wakivuta mkia wa jedwali bila alama yoyote ligini.Norwich almaarufu The Canaries sasa ndicho kikosi cha nne katika historia kuwahi kupoteza mechi tano mfululizo za ufunguzi wa msimu wa EPL huku kocha wao Daniel Farke akiwa wa kwanza kupoteza mechi 15 mfululizo za EPL.

Kwa ushindi wao ambao ulikuwa wa pili msimu huu, Watford walipaa hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo wa jedwali. Emmanuel Dennis alimzidi ujanja beki Ozan Kabak na kufungia Watford bao la kwanza kutokana na krosi ya Kiko Femenia.

Ingawa Teemu Pukki alikamilisha krosi ya Mathias Normann na kumwacha hoi kipa Ben Foster katika tukio lililotarajiwa kurejesha Norwich mchezoni, kikosi hicho Sarr aliwaweka Watford uongozini baada ya kumbwaga kipa Tim Krul.

Bao la Pukki lilitamatisha ukame wa mabao wa nyota huyo raia wa Finland aliyekuwa hajafunga goli lolote isiyotokana na penalti kuanzia 2019.Mechi hiyo ilikutanisha vikosi viwili vilivyopandishwa ngazi kunogesha soka ya EPL miezi miwili baada ya kuteremshwa daraja.

Ingawa Farke alisaidia Canaries kurejea EPL, kushindwa kwao katika msururu wa mechi nyingi zikiwemo 10 za mwisho katika msimu wa 2019-20 ndiyo rekodi mbovu zaidi kwa kocha yeyote ya EPL kuwahi kushuhudia.

Watford walifanyia kikosi chao mabadiliko manne huku Norwich wakifanyia kikosi chao mabadiliko matano.Hata hivyo, wanasoka wote wanne wapya wa Watford walikuwa katika miaka yao ya 30, kila mmoja akiwa mwingi wa tajriba, akiwemo kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Ben Foster.

Norwich walichezesha Kabak na Normann kwa mara ya kwanza huku Josh Sargent akiwajibishwa kwa mara ya kwanza katika EPL. Kila kikosi kilivurumisha makombora 12 huku Norwich wakitamalaki dakika 15 za kwanza katika kipindi cha pili.

  • Tags

You can share this post!

Mane afikisha mabao 100 akivalia jezi za Liverpool

Aston Villa yapiga Everton breki kali kwenye EPL