• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Man-City wapoteza pointi mbili muhimu za EPL dhidi ya Southampton ugani Etihad

Man-City wapoteza pointi mbili muhimu za EPL dhidi ya Southampton ugani Etihad

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City walipoteza alama mbili muhimu katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kulazimishiwa sare tasa na Southampton mbele ya mashabiki 53,500 ugani Etihad.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City walikosa kuelekeza kombora lolote langoni mwa Southampton hadi dakika ya 90. Mabingwa hao watetezi wa EPL walishindwa kutamba jinsi ilivyotarajiwa huku ushirikiano kati ya viungo na mafowadi ukikosa kabisa kuonekana.

Burnley walipewa mkwaju wa penalti katika dakika ya 60 baada ya beki Kyle Walker kuonyeshwa kadi nyekundu kwa tukio la kumchezea visivyo Adam Armstrong ndani ya kijisanduku.

Hata hivyo, maamuzi hayo yalibatilishwa na teknolojia ya VAR baada ya refa Jon Moss kuirejelea.Nusura Armstrong awaweke Southampton kifua mbele katika dakika ya 70 ila ikabainika kwamba alimchezea Walker visivyo.

Man-City walidhani walikuwa wamefunga bao la ushindi mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Raheem Sterling kufuatiliza mpira wa kichwa uliopigwa na Phil Foden. VAR ilichangia kudumishwa kwa maamuzi ya awali ya Man-City kunyimwa penalti kwa madai kwamba Sterling alikuwa ameotea.

Kwa matokeo hayo, Southampton kwa sasa hawajashinda mechi yoyote ya EPL hadi kufikia sasa baada ya kuambulia sare mara nne kutokana na mechi tano zilizopita. Kwa upande wao, Man-City kwa sasa wameachwa na Liverpool kwa pointi tatu zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Aston Villa yapiga Everton breki kali kwenye EPL

Arsenal wacharaza Burnley na kupunguzia Arteta presha ya...