• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Bei ya juu ya gesi yasukuma Wakenya kukumbatia makaa, kuni

Bei ya juu ya gesi yasukuma Wakenya kukumbatia makaa, kuni

Na KENYA NEWS AGENCY

IDADI kubwa ya Wakenya sasa wamelazimika kutumia kuni tena kupika vyakula kufuatia kuongezwa kwa bei ya gesi miezi miwili iliyopita.

Serikali ilianza kutoza gesi ushuru wa asilimia 16 wa thamani ya ziada (VAT) baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuidhinisha Mswada wa Fedha wa 2020 mnamo Juni 2020.

Ushuru huo wa VAT, ulifaa kuanza kutozwa mwaka 2020 lakini uliahirishwa hadi mwaka huu wa 2021.

Ushuru huo ulisababisha bei ya mtungi wa gesi wa kilo 13 kupanda hadi Sh2,600 kutoka Sh2,000.

Bei ya mtungi wa kilo 6 iliongezeka hadi Sh1,200 kutoka Sh900.

Bi Mary Atieno ambaye amekuwa akitumia gesi kupika chakula katika kibanda chake katika eneo la Free Area mjini Nakuru, anasema kuwa amelazimika kuongeza bei ya chakula kuepuka hasara.

“Nimelazimika kupandisha bei ya chakula ili kuepuka hasara – hali ambayo imesababisha wateja kupungua. Nitaanza kutumia makaa ili nisije nikapoteza wateja wangu,” alisema Bi Atieno.

Tangu 2016, Wakenya wamekuwa wakifurahia bei ya chini ya gesi ya kupikia baada ya Wizara ya Fedha kufutilia mbali ushuru wa VAT wa bidhaa hiyo.

Bi Caroline Nyokabi, mkazi wa Karatina, Kaunti ya Nakuru alisema kuwa amelazimika kutumia kuni kutokana na gharama ya juu ya gesi.

“Kwa miezi miwili sasa sijakuwa nikitumia gesi kupika kwani siwezi kumudu bei ya juu. Kwa sasa natumia kuni kupika chakula,” akasema Bi Nyokabi.

You can share this post!

Mke amhadaa mumewe kuwa alitekwa

Suarez afunga mabao mawili na kusaidia Atletico Madrid...