• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Abiria kutumia reli kutoka Mombasa hadi Malaba kuanzia Novemba

Abiria kutumia reli kutoka Mombasa hadi Malaba kuanzia Novemba

MACHARIA MWANGI na ERIC MATARA

SAFARI kati ya Mombasa na Malaba mpakani mwa Kenya na Uganda, kwa kutumia treni, zitaanza Novemba, mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli nchini Philip Mainga, alifichua kuwa shughuli ya kuunganisha Reli ya Kisasa (SGR) na reli ya zamani katika eneo la Longonot, imekamilika.

Hiyo inamaanisha kuwa Wakenya wanaotaka kusafiri kati ya Mombasa, Nairobi, Kisumu na Busia kwa ajili ya sherehe za Krismasi watatumia treni.

“Safari za treni kati ya Nairobi na Malaba zitaanza Novemba kupitia reli iliyokarabatiwa,” Bw Mainga akasema. Ijumaa, Bw Mainga aliandamana na Kamati ya Bunge kuhusu Fedha kuzuru kituo cha reli cha Naivasha.

Uchunguzi uliofanywa na Taifa Leo ulibaini ujenzi wa eneo la umbali wa kilomita 23.5 linalounganisha SGR na reli ya zamani katika eneo la Longonot umekamilika.

Ujenzi wa eneo hilo kati ya Maai Mahiu na Longonot ulianza Agosti mwaka jana.Shirika la Reli pia limejenga kituo cha mizigo na abiria katika eneo la Longonot.

Reli ya zamani iliyokarabatiwa inatarajiwa kuboresha shughuli za kibiashara katika miji inayopitia kati ya Nakuru na Kisumu.

You can share this post!

Kilio familia 89 Kwale zikihofia kufurushwa

TAHARIRI: Serikali isilazimishe walimu kusoma tena