Habari Mseto

Aachiliwa baada ya kuishi rumande siku 15

March 25th, 2020 1 min read

NA RICHARD MUNGUTI

Baada ya kukaa rumande kwa siku 15, mlinzi Spencer Kipkorir alipata afueni alipoachiliwa na hakimu mwandamizi Kennedy Cheruiyot Jumatano.

Wakili Ham Kiplagat aliyemwakilisha Spencer alieleza mahakama kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma hajafikia uamuzi ikiwa atamfungulia mashtaka mshukiwa huyo au la.

“Afisa anayechunguza kesi dhidi ya mshukiwa hajakamilisha zoezi hilo kwa vile chuo kikuu cha Nairobi kinefungwa na mashahidi,” kiplagat aliambia hakimu.

Aliomba mshukiwa aachiliwe kwa dhamana akiongeza” siku ile uchunguzi utakamilika DPP ataamua ikiwa atamfungulia mashtaka.”

Wakili Ham Langat (kushoto) akiwa na Kipkorir nje ya mahakama ya Milimani. Picha/ Richard Munguti

Akitoa uamuzi Bw Cheruiyot alisema mashahidi hawajapatikana na mshukiwa hawezi zuiliwa hadi wakati ule mashahidi watakapopatikana.

Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh1milioni moja pesa tasilimu.

Bw Cheruiyot alimwamuru mshhkiwa huyo aripoti kila siku kwa afisa anayexhunguza kesi hiyo katika kituo cha polisi cha Kilimani hadi uamuzi wa kumfungulia mashtaka utakapochukuliwa na DPP.

Bw Cheruiyot alisema madai yanayomkabili mshukiwa huyu ni makali kwa vile mwanafunzi wa chuo kikuu alipoteza maisha.