Habari Mseto

Abambwa akisafirisha bandi ya mamilioni

November 18th, 2020 1 min read

NA BRUHAN MAKONG

Polisi mjini Wajir walikamata mwanamume aliyekuwa akisafirisha bangi yenye thamani ya  Sh1.75 milioni.

Mshukiwa aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser alikamatwa Ijumaa baada ya wakazi kujulisha polisi.

Naibu wa Kamanda wa polisi wa eneo la  Eldas Vincent Lomachar alisema kwamba mshukiwa huyo alikuwa akiendesha gari kutoka Moyale akielekea Isiolo.

“Hili ni tukio la tatu kutokea eneo hilo tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Walanguzi wa dwa za kulevya utumia njia hiyo ili wahepe maafisa wa usalama ,”alisema Bw Laomachar.

Aliogeza kwamba washukiwa hao watafikishwa kortini Jumatatu. Aliwaomba wakazi kama wanahabari zozote kuhusiana na hayo wakisite kuwajulisha polisi.

“Tunaomba wakazi wawachunguze watu akma hao na wafanye kazi na maafisa wa usalama ili kuakikisha kwamba biashara hiyo haramu imesimamishwa,”aliogeza.

Bw  Lomachar alisema kwamba maafisa wa usalama wanafanya njuu chini ili kusimamisha matukio kama hayo.

Walanguzi wengi wa madawa za kulevya huingia humu nchini kupitia maeneo hayo kutoka nchi jirani ya Ethiopia.

Tafsiri na Faustine Ngila