Habari Mseto

Abambwa baada ya kumuua mwanawe

June 7th, 2020 1 min read

NA WYCLIFFE NYABERI

Polisi katika Kaunti ya Nyamira walimkamata jamaa mmjoja kwa kosa la kumuua mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 4 Jumapili.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 40 anaaminika kutenda kitendo hicho baada ya mkewe kumkataza kulala kitanda moja na mwanawe wa kike.Tukio hilo lilitotokea kwenye Kijiji cha Nyakeremera eneo la Itibo Nyamira Kaskazini.

Kamishna wa kaunti hiyo Amos Mariba lisema kwamba mshukiwa alikuwa ametofautiana na mkewe baada ya mwanaume huyo kutaka kulala kitanda moja na mtoto wake wa kike kitu saa tatu asubuhi.

Mwanaume huyo alimpiga mwanawe kwa kifaa butu huku msichana huyo akiaga dunia papo hapo. Baada ya kumuua mwanawe alimgeukia bibi yake akampiga na kumwacha na majeraha.

“Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Kaunti hiyo,” alisema Mariba.

Haikueleweka ni kwa nini jamaa huyo aliamua kumuua mwanawe lakini jirani wa karibu alisema kwamba mke wa jamaa huyo alishuku kuwa mwanamume huyo angemdhulumu kimapenzi msichana huyo.

Huku visa vya ubakaji vikiendelea kuongezeka kwenye kaunti hiyo mwanmke huyo alishuku lengo la bwanake kutaka kulala kitanda moja na mwanawe.