Dondoo

Abwaga mpenzi aliyekosa kumnunulia gari Valentino

February 15th, 2018 1 min read

 Na JOHN MUSYOKI

KATULYE, MASINGA

MWANADADA  kutoka sehemu hii, alitokwa na machozi baada ya mpenzi wake kumpiga chenga na kukataa kumtimizia ahadi siku ya wapendanao.

Inasemekana jamaa alikuwa amemuahidi  gari siku ya wapendanao mwaka huu.

Kwa furaha, demu alizidisha mapenzi kwake. Hata hivyo siku ilipowadia, jamaa aliingia mitini.Inasemekana demu aliamua kwenda kumtafuta na akampata akitulia kwake.

“Nimesubiri zawadi kwa muda mrefu hadi siku imefika. Uliniahidi  gari na sasa haushughuliki,” demu alisema.  Inasemekana jamaa alimweleza hakuwa na pesa na demu akaanza kufoka.

“Wewe ni mtu muongo sana. Kama hauwezi kutimiza ahadi utaweza kunilisha ukinioa?” demu alisema akilia kisha akamtema jamaa huyo.