AC Milan wapepeta Bologna katika Serie A licha ya Zlatan Ibrahimovic kupoteza penalti

AC Milan wapepeta Bologna katika Serie A licha ya Zlatan Ibrahimovic kupoteza penalti

Na MASHIRIKA

ZLATAN Ibrahimovic alipoteza mkwaju wa penalti katika mchuano wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) iliyoshuhudia waajiri wake AC Milan wakisajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Bologna na kufungua mwanya wa alama tano kileleni mwa jedwali.

Ibrahimovic aliyepigwa marufuku ya mechi moja kwenye kipute cha Coppa Italia mnamo Januari 29 kwa utovu wa nidhamu alipovurugana na Romelu Lukaku wa Inter Milan kwenye mchuano wa awali, alinyimwa penalti na kipa Lukasz Skorupski wa Bologna kabla ya Ante Rebic kufunga.

Franck Kessie alifunga bao la pili la Milan ambao chini ya kocha Andrea Poli, wanajivunia alama 46, saba zaidi kuliko mabingwa watetezi Juventus waliowapokeza Sampdoria kichapo cha 2-0 katika mechi nyingine ya Jumamosi usiku.

Nusura Roberto Soriano asawazishie Bologna mwishoni mwa kipindi cha kwanza ila juhudi zake zikazimwa na kipa Gianluigi Donnarumma.

You can share this post!

Dortmund wacharaza Augsburg na kukomesha ukame wa mechi...

Kutimuliwa kwa kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kuna athari...