AC Milan wapoteza fursa ya kutua kileleni mwa jedwali la Serie A

AC Milan wapoteza fursa ya kutua kileleni mwa jedwali la Serie A

Na MASHIRIKA

AC Milan walipoteza fursa ya kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya utepetevu wao kuruhusu Sassuolo kutoka nyuma na kuwapepeta 3-1 mnamo Jumapili uwanjani San Siro.

Nahodha Alessio Romagnoli aliwaweka Milan kifua mbele katika dakika ya 21 kabla ya Sassuolo kusawazisha dakika tatu baadaye aliposhirikiana vilivyo na Gianluca Scamacca.

Simon Kjaer wa Milan alijifunga katika dakika ya 33 kabla ya Domenico Berardi kupachika wavuni bao la tatu la Sassuolo. Milan walikamilisha mechi na wanasoka 10 pekee uwanjani baada ya Romagnoli kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumkabili Gregoire Defrel visivyo mwishoni mwa kipindi cha pili.

Milan ambao kwa sasa wametandaza mechi tatu mfululizo bila kushinda yoyote katika Serie A, wanashikilia nafasi ya pili kwa alama 32, tatu zaidi nyuma ya viongozi Napoli waliowaponda Lazio 4-0.

Ushindi wa Sassuolo ulikuwa wao wa kwanza baada ya michuano minne ligini.

MATOKEO YA SERIE A (Jumapili):

AC Milan 1-3 Sassuolo

Roma 1-0 Torino

Napoli 4-0 Lazio

Udinese 0-0 Genoa

Spezia 0-1 Bologna

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Oboya Cup: Susa, Rongai zatua nusu fainali

PSG wazamisha St-Etienne na kufungua pengo la alama 12...

T L