Achani azindua kampeni dhidi ya Ukimwi

Achani azindua kampeni dhidi ya Ukimwi

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI ya kaunti ya Kwale imezindua kampeni kuhamasisha wakazi dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Serikali hiyo inayoongozwa na Gavana Fatuma Achani inalenga watu 1,000 kwenye kampeni hiyo katika wilaya nne za Kwale.

“Kampeni hii ni muhimu sana ambayo inalenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kaunti ya Kwale,” alisema Bi Achani alipozindua kampeni hiyo katika ukimbi wa Kwale Cultural Centre.

Takwimu zinaonyesha asilimia 3.2 ya wakazi wa Kwale wameambukizwa Ukimwi. Idadi kubwa ya waathiriwa ni vijana.

  • Tags

You can share this post!

Masharti makali ya kutoshiriki ngono waliopona Ebola

Arsenal wakomoa Spurs ugani Emirates na kufungua pengo la...

T L