Habari Mseto

Adai haelewi shtaka la kuuza lori la mamilioni kabla ya kulilipia

December 4th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MMILIKI wa lori lenye thamani ya Sh5.4milioni aliyeliuza kabla ya kukamilisha kulipa mkopo wa benki ameshtakiwa.

Shadrack Savali Mwobami alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi Muthoni Nzibe katika Mahakama ya Milimani Nairobi.

Mahakama ilifahamishwa mshtakiwa aliuliza lori hilo kwa bei ya Sh5,469,750 ilhali alijua hajakamilisha kulipa mkopo wa Housing Finance (HFC).

Lori hilo lilikuwa nambari KCG muundo wa Isuzu FSR.

Mahakama ilielezwa mshtakiwa aliuliza liro hilo kati ya Januari 28, 2016 na Novemba 29 2019.

Aliposomewa shtaka mshtakiwa aliambia korti hakuelewa hata ikabidi karani wa mahakama amsongee karibu kumweleza kwa lugha ya Kiswahili.

Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya Sh3 milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.