Adai kortini akivuta bangi huongeza nguvu za kiume

Adai kortini akivuta bangi huongeza nguvu za kiume

Na TITUS OMINDE

SHAMBABOI alisababisha kicheko katika mahakama ya Eldoret alipodai uvutaji bangi humpa nguvu na uwezo wa kutekeleza majukumu yote, likiwemo la tendo la ndoa.

Korti iliambiwa Peter Asieche alikamatwa mnamo Mei 15 katika eneo la Flax, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, akiwa na gramu 100 za bangi ya thamani ya Sh2,000.

“Mimi si mfanyabiashara wa dawa za kulevya lakini ni mvutaji sugu. Uvutaji bangi hunipa nguvu za kutekeleza majukumu ikiwa ni pamoja na kumtunza vizuri mke wangu na watoto,” alimwambia hakimu mwandamizi mkuu wa Eldoret, Bi Naomi Wairimu.

Alitozwa faini ya Sh5,000 au atumikie kifungo cha miezi mitano jela.

You can share this post!

USANII MASHINANI: Msanii na mtangazaji wa runinga, studio...

Arsenal wacharaza Crystal Palace ugenini na kupaa hadi...