Habari Mseto

Adungwa kisu cha kifo kwenye mzozo kilabuni

October 20th, 2020 1 min read

NA AMINA WAKO

Mwanamume mmoja alidungwa kisu hadi kifo alipokuwa kwenye kilabu kimoja mji wa Kehancha Kuria Magharibi Kaunti ya Migori.

Kulingana na ripoti za polisi tukio hilo lilitokea Oktoba 17,2020 ambapo Bw Frenk Nyandoto alidungwa kisu na Julius Mohere.

Wawili hao walianza kupigana walipokuwa ndani ya kilabu cha Annex kabla ya kutolewa nje.

Bawabu wa klabu hiyo Chacha Matiko Masaga aliaambia polisi kwamba walipotolewa njeewawili hao waliendelea kutupiana maneno makalii.

“Wawili hao walianza kurushiana maneno juku wakikaribiana hapo ndipo Nyandoto alimdunga kisu Mohere tumboni akitumia kisu  naa akatoroka,”zilisema ripoti za polisi.

Kulingana na bawabu huyo mwendazak alikimbia kuelekea kwa lango kuu huku akiomba usaindizi akishikilia matumbo yake yaliokuwa yametoka nje.

Alikimbizwa hospitali ya Kuria Magharibi alipofariki na mwili wake kupelekwa kwenye chumba cha  kuhifadhi maiti cha hospitali ya Migori.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA