Habari Mseto

Afariki baada ya kukosa hewa timboni

June 27th, 2020 1 min read

NA LUCY MKANYIKA

Mtu mmoja amefariki na mwingine kulazwa hospitalini baada ya kuzimia kwa kukosa hewa ya kupumua katika timbo moja eneo la Mwatate kaunti ya Taita Taveta.

Mwili wa mtu huyo ulipatikana kwenye timbo la Mkuki na wenzake Jumanne jioni waliokuwa wakichimba mawe timboni humo,

Mwenyekiti wa muungano wa wachimbaji wa mawe wa Mkuki Reuben Mwawughanha alisema kwamba mtu huyo wa pili aliyeokolewa alipelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Moi Voi kwa matibabu.

Bw Mwawughanga alisema wawili hao walikuwa wakitoa maji kwenye timbo hilo wakati tukio hilo lilitokea.

“Tulirejea kazini hivi karibuni baada ya kufunga kwa miezi miwili baada ya serikali kuangiza kufungwa kwa matimbo ya uchimbaji mawe ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. Wakati hatukuwa tunafungua timbo hilo liliingia maji ya mvua. Wachimbaji walikuwa wanatoa maji iliwarejee kazini,” alieleza.

Huku akithibitisha hayo Naibu Kamishena wa kaunti hiyo Damaris Kimondo alisema wachimbaji migodi hao waliokolewa na kukimbizwa hospitali ambapo mmoja alitangazwa kuwa amefariki.

Mwaka uliopita wachimbaji wengine watatu walifariki baada ya kufunikiwa ndani ya timbo la Kasigau kaunti ndogo ya Voi.

Tafsiri: Faustine Ngila