Michezo

AFCON: Ahmed Musa na Shehu watua Nigeria

June 5th, 2019 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

MARA tu baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, nyota wawili Ahmed Musa na Abdullahi Shehu wamewasili Asaba, Nigeria kujinoa na kikosi cha Super Eagles.

Kadhalika, mshambuliaji Alex Iwobi wa Arsenal aliwasili na kwenda moja kwa moja Golden Tulip Hotel muda mfupi kabla ya timu hiyo kuandaliwa chakula cha mchana. Mshambuliaji matata Odion Ighalo aliyeongoza kwa mabao msimu huu alitarajiwa kufika saa chache baadaye.

Mabingwa hao mara tatu wanaendelea kujinolea Asaba kwa ajili ya kupimana nguvu na Zimbabwe, Vijana hao wa kocha Gernot Rohr wanatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Senegala, Jumapili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Misri kushiriki fainali za Afcon.

Ni mlinzi William Ekong pekee anayetarajiwa kufika Ahamisi.

Kikosi cha Nigeria kitasafirishwa Jumapili usiku kwa ndege maalum hadi nchini Misri kwa maandalizi mengine makali Nigeria.

Chama cha Soka Nigeria (NFF) kimepewa hadi Jumanne kuwasilisha CAF majina ya wachezaji.