Michezo

AFCON: Ghana yatuma mashabiki 100 Cairo

June 5th, 2019 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

Serikali ya Ghana itagharamia mashabiki 100 kwenda nchini Misri kushangilia timu ya taifa, The Black Stars wakati wa mechi zao za Afcon.

Kwenye mechi hizo, Black Stars imepangiwa katika Kundi F pmaoja na Benin, Cameroon, na Guinea-Bisau ambapo itaanza kucheza dhidi ya Guinea- Bisau

Mwenyekiti wa Muungano wa Mashabiki Ghana, Abraham Boakye maarufu kama “one man supporter” alifichua habari hizo baada ya kujulishwa na serikali.

Kupitia kwa kituo cha redio jana, shabiki huyo maarufu alisema watakaokuwa ziarani humo ni wale wanaotambuliwa kwa kushangilia timu hadi dakika ya mwisho.