Michezo

AFCON: Zimbabwe kupasha misuli joto dhidi ya Nigeria

June 5th, 2019 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

Kikosi cha wanasoka 26 cha timu ya taifa ya Zimbabwe maarufu kama Warriors, kitatua nchini Nigeria Alhamisi kwa ndege ya Shirika la Ndege Afrika Kusini ambapo Jumamosi kitakabiliana na Super Eagles ya Nigeria katika mechi ya kimataifa ya kupimana nguvu.

Baada ya kutua, kikosi hicho kitabakia jijini Lagos na badaye Ijumaa kuondoka asubuhi hadi Asaba itakakochezewa mechi hiyo ya kirafiki, itakayochezewa Stephen Keshi Stadium.

Zimbabwe wamepangiwa katika Kundi A la michuano yam waka huu ya kuwania ubingwa wa Afcon, Makala ya 32 itakayofanyika nchini Misri kati ya Juni 21 na Julai 19.

Wamo katika kundi moja pamoja na wenyeji Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda Cranes. Nigeria imo katika Kundi B pam oja na Burundi, Guinea na Madagascar.

Warriors wataanza dhidi ya Egypt ugani Cairo Stadium mnamo Juni 21.