Michezo

#AFCON2019: Harambee Stars yaanza kunoa kucha

May 20th, 2019 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kenya wameanza Jumatatu maandalizi yao ya Kombe la Bara Afrika (AFCON) litakalofanyika nchini Misri kutoka Juni 21 hadi Julai 19, 2019.

Kocha Sebastien Migne na vijana wake walifanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Wachezaji 18 walihudhuria kipindi hicho cha kwanza cha mazoezi, wengi wao wakiwa kutoka ile timu itakayoshiriki mechi za kufuzu za Soka ya Bara Afrika ya wachezaji wanaosakata katika mataifa yao almaarufu CHAN.

Musa Mohammed, Cliffton Miheso, Dennis Odhiambo na Masoud Juma ni baadhi ya wachezaji walioitwa katika kikosi cha AFCON waliojitokeza kwa mazoezi hayo ya kwanza.

Harambee Stars, ambayo inarejea katika AFCON baada ya kuwa nje miaka 15, itaelekea nchini Ufaransa hapo Mei 31 kwa matayarisho kabambe ya wiki tatu. Stars itakita kambi jijini Paris kwa siku 19 kabla ya kuelekea nchini Misri mnamo Juni 19.

Jijini Paris, Stars pia itasakata mechi mbili za kirafiki dhidi ya Madagascar (Juni 7) na Gambia (Juni 15).

Kenya itaanza kampeni yake ya AFCON dhidi ya Algeria mnamo Juni 23 uwanjani 30 June Stadium jijini Cairo. Itakutana na Tanzania (Juni 27) na Senegal (Julai 1) katika mechi zingine za Kundi C.

Katika kampeni ya kufuzu kushiriki CHAN kwa mara ya kwanza kabisa, Kenya itakabiliana na Burundi mwezi Agosti. Mshindi kati yao atajikatia tiketi ya kulimana na Tanzania ama Sudan katika awamu ya mwisho ya kufuzu ambayo mshindi ataingia CHAN itakayoandaliwa nchini Ethiopia mwezi Januari mwaka 2020.

Orodha ya wachezaji walioshiriki kipindi cha kwanza cha mazoezi (Mei 20):

Makipa – John Oyemba, Brian Bwire

Mabeki – David Ochieng’, Charles Momanyi, Eric Juma, Musa Mohammed, Mike Kibwage;

Viungo – Dennis Odhiambo, Joe Waithira, Teddy Osok, Duke Abuya, Cliffton Miheso, Ibrahim Shambi, Paul Were;

Washambuliaji – John Avire, Enosh Ochieng, Pistone Mutamba, Masud Juma

Kikosi kizima cha Kenya:

AFCON

Makipa

Patrick Matasi, Farouk Shikalo, John Oyemba, Brian Bwire

Mabeki

David Owino, Brian Mandela, Musa Mohammed, Bernard Ochieng, Joseph Okumu, Joash Onyango, Eric Ouma, Aboud Omar, Philemon Otieno

Viungo

Victor Wanyama, Ismael Gonzalez, Athony Akumu, Dennis Odhiambo, Johanna Omollo, Francis Kahata, Paul Were, Eric Johanna, Clifton Miheso, Ovella Ochieng, Ayub Timbe, Whyvhonne Isuza

Washambuliaji

Michael Olunga, Masoud Juma, Christopher Mbamba, John Avire, Allan Wanga

CHAN

Makipa

Farouk Shikalo, John Oyemba, Brian Bwire

Mabeki

Philemon Otieno, Joash Onyango, Bernard Ochieng, Charles Momanyi, Michael Kibwage, Andrew Juma, David Ochieng, David Owino, Eric Juma

Viungo

Roy Okal, Teddy Osok, Patillah Omotto, Dennis Odhiambo, Ibrahim Shambi, Duke Abuya, Whyvonne Izusa, Cliff Nyakeya, Kenneth Muguna, Francis Kahata, Samuel Onyango, Paul Were, Abdalla Hassan, Joe Waithera

Washambuliaji

John Avire, Sydney Lokale, Nicholas Kipkirui, Piston Mutamba, Allan Wanga, Enos Ochieng