Michezo

AFCON2023: Ivory Coast na Nigeria wamwagia wachezaji mamilioni na nyumba za kifahari

February 21st, 2024 2 min read

NA JOHN ASHIHUNDU

MARAIS wa nchi za Ivory Coast na Nigeria wametoa pongezi na zawadi nono za mamilioni ya pesa pamoja na nyumba kwa wachezaji waliowezesha timu za nchi hizo kutinga fainali ya Afcon iliyochezwa Februari 11, 2023 ugani Alassane Quattara Stadium.

Mbali na pongezi hizo, vile vile kila mchezaji kwenye timu hizo alipokea mamilioni ya pesa pamoja na nyumbani kifahari.

Baada ya kushinda Nigeria kwa 2-1 fainalini, kila mchezaji wa Ivory Coast amepokea Sh12 milioni na nyumba ya thamani ya kiasi hicho cha pesa.

Akitoa tuzo hizo, Rais Alassane Quattara aliwapongeza wachezaji hao kwa kuletea taifa sifa hizo za kimataifa katika mashindano hayo ya aina yake ambayo yalishuhudiwa na zaidi ya watu bilioni mbili kote duniani, idadi ambayo ni kubwa zaidi katika historia ya miaka 67 ya mashindano hayo.

Soma pia Ivory Coast ‘walivyobahatika’ kufika nusu fainali ya AFCON 2023, ndivyo watabeba Kombe?

Nchini Nigeria, rais Bola Tunubu alitoa Sh7.5 milioni kwa kila mchezaji, nyumba ya kifahari mjini Abuja pamoja na shamba karibu na jiji hilo kwa kila mmchezaji.

Kwa ushindi huo, tayari Ivory Coast ilikuwa imepokea zaidi ya Sh1 bilioni kutoka kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (Afcon) wakati Nigeria ikipata Sh582 milioni.

Afrika Kusini na DR Congo kila moja ilipokea zaidi ya Sh363 milioni, wakati kila timu iliyotinga hatua ya robo-fainali ilipata Sh189 milioni. Afrika Kusini ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kushinda DR Congo kwa 6-5 kupitia mikwaju ya penalti.

Kulingana na orodha ya viwango vya Shirikisho la Kimataifa vya FIFA iliyotolewa Alhamisi, Ivory Coast na Nigeria zimepiga hatua kubwa baada ya kumalizika kwa Afcon.

Soma pia Ni fainali ya ‘Oga’ kumla ‘Ndovu’ dimba la AFCON

Ivory Coast imepanda nafasi 10 kwenye orodha hiyo hadi nafasi ya 39, Nigeria ikiruka mara 14 hadi nafasi ya 28, licha ya kushindwa fainalini.

Angola ndio iliyofaidika zaidi kwa kuruka hadi nafasi ya 93 baada ya kuruka nafasi 14, wakati Tunisia na Algeria zikishuka hadi nafasi za 41 na 43 mtawalia.

Morocoo inaendelea kuongoza kwa mataifa ya Afrika ikiwa katika nafasi ya 12, licha ya kubanduliwa katika hatua ya 16-Bora katika Afcon.

Senegal inashikilia nafasi ya 17, wakati Argentina ikiendelea kuongoza msimamo huo wa kimataifa, mbele ya Ufaransa na Uingereza.

Soma pia VAR yaongeza ladha ya Afcon