Afisa afungwa miaka 100 kwa kulawiti watoto

Afisa afungwa miaka 100 kwa kulawiti watoto

NA RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa makao ya watoto amefungwa miaka 100 kwa kuwalawiti wavulana wa umri mdogo.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mwandamizi wa mahakama ya Milimani, Bi Zainabu Abdul, alisema Stephen Nzuki Mutisya mwenye umri wa miaka 29 alikuwa ananukuu vifungu vya Biblia akiwadanganya vijana hao kwamba kitendo hicho kinakubaliwa na Mungu.

“Mshtakiwa alikuwa anajifanya Mkristo kumbe alikuwa na nia mbovu ya kuwafundisha wavulana tabia isiyokubalika katika jamii,” alisema Bi Abdul.

Hakimu huyo alisema kitendo hicho ni kibaya mno na kinakiuka haki za wavulana hao waliokuwa wa umri kati ya miaka minne na sita.

Bi Abdul alisema mshtakiwa anapaswa kutengwa na watoto pamoja na wanawake.

Aliongeza kuwa mahakama zina mamlaka ya kuwatunza wavulana, wasichana na watu katika jamii walio na changamoto za kiafya.

“Mahakama hii imekupata na hatia na utatumikia kifungo cha miaka 100 gerezani,” aliamuru Bi Abdul.

Hakimu huyo alisema wahasiriwa waliomba mahakama imwadhibu vikali kwa kuwa aliwatumia vibaya na kukandamiza haki zao.

Alitenda uhalifu huo kati ya 2010-2016.

  • Tags

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Kutofaa kwa matumizi ya ‘iko’ kwa maana...

Raila ashinda kesi kuhusu utumizi wa daftari

T L