Michezo

Afisa aisifia Safaricom kuandaa kipute cha Chapa Dimba

April 29th, 2019 2 min read

Na JOHN KIMWERE

KUSEMA kweli Safaricom inapiga shughuli safi. Ni matamshi yake kinara wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Tawi la Nairobi West, Bashir Hussein akiipongeza wakati wa fainali za Chapa Dimba na Safaricom Season Two Mkoani Nairobi.

Afisa huyo ametoa mwito kwa serikali za Kaunti kuiga mtindo huo kama ilivyo katika mataifa mengine kama Ghana na Nigeria.

Pia ameyataka mashirika mengine nchini Coca Cola bila kuweka katika kaburi la sahau kiwanda cha kutengeneza mvinyo cha Kenya Breweries kuwazia namna yanavyoweza kusaidia vijana chipukizi.

”Ningependa kutaja kwamba milango iwaza kwa mashirika ya humu nchini kufkanya kazi na maofisa wa FKF ili kukuza talanta za wachezaji chipukizi wavulana na wasichana,” alisema na kuongeza kuwa shirikisho hilo limo chini ya viongozi wapya wasiopenda kushiriki ufisadi.

Kadhalika alielezea kuridhishwa kwake na jinsi Safaricom alivyoendesha mechi za makala ya pili ambazo fainali za kitaifa zitafanyika mwezi Juni kule Kinoru Stadium, Kaunti ya Meru.

Ofisa huyo alisema serikali za Kaunti zinastahili kujenga angalau uwanja mmoja wa hadhi ya juu katika kila kaunti kwa ajili ya wachezaji chipukizi kufanyia mazoezi.

Ofisa wa kamati kuu, FKF Chris Amimo (kati) akizungumza na ofisa wa FKF, Nairobi West, Bashir Hussein (kulia) na katibu wa tawi hilo Caleb Malweyi wakati wa fainali za Chapa Dimba na Safaricom Season Two Mkoani Nairobi. Picha/ John Kimwere

Pia kutumika wakati wa mashindano ya mechi hizo ambazo huendeshwa na Safaricom pia Coca Cola.

”Mwaka huu tumeshuhudia michezo bora zaidi tofauti na mwaka uliyopita hali inayoashiria wazi kwamba wachezaji wanatambua umuhimu wa kukuza talanta zao,” alisema.

Aidha alipongeza jinsi shughuli za michezo ya mwaka huu zilivyopangwa huku akisifia mtindo uliotumiwa kuteua wachezaji wa timu za taifa wavulana na wasichana.

Waliohusika na zoezi hilo walinasa mchezaji bora katika maeneo yote nane kote bila ubaguzi, shughuli iliyopenda wengi wakimo wachezaji wanaokuja.

”Bila kipendeleo uteuzi huo unawatia motisha wachezaji wenzao na kuamini wakitia bidii nao pia watakuwa pazuri kuteuliwa kuwakilisha timu za taifa. Chipukizi 16 wavulana sawa na wasichana waliteuliwa kwa katika timu za taifa ambapo wiki ijayo watasafiri nchini Uhispania kushiriki maezoezi ya soka dhidi ya wenzao wanaoshiriki Ligi ya Laliga.

Kadhalika alitoa mwito kwa wazazi ambao wanao hushiriki mchezo wowote wawe wakianza kushughulikia masuala ya visa vya kusafiri katika mataifa ya kigeni mapema. Alidokeza kwamba wapo wachezaji walioteuliwa kujiunga na vikosi hivyo lakini hawatakuwa katika ziara hiyo maana hawana pasipoti.