Habari Mseto

Afisa wa DCI azimwa kumumunya hongo

August 24th, 2020 1 min read

NA MOHAMED AHMED

Afisa wa DCI ametiwa baroni Mombasa kwa kuchukua pesa kutoka kwa mwananchi kwa kutumia udanganyifu.

Konstebo huyo wa polisi Bw Edward Mwaniki kutoka kituo cha polisi cha Kisauni anasemaka kuchukua pesa kutoka kwa mwanamke mmoja n kumuhaidi kwamba angetafutia jmaa zake kazi.

Pesa ambazo alisemekana kuchukua hazikutajwa kiasi chake. Kulingana na ripoti ya polisi afisa huyo alijifanya kuwa na uwezo wa kupeana kazi wakati wa kuajiriwa kwa maafisa wa magereza 2017.

“Kukamatwa kwake kulijiri baada ya DCI wa Likoni kusema akamatwe na kushtakiwa kwa kuchukua pesa kwa udanganyifu,”alisema DCI.

Bw Kabachia anasemekana kuhusika na mbwa za usalama za Kisauni na amekuwa akifanya kazi kwenye korti za Mombasa.

Amekuwa akiendesha kesi kwenye kituo cha polisi cha Kisauni kama kama afisa wa uchunguzi.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA