Afisa wa ODM apatikana na Covid-19

Afisa wa ODM apatikana na Covid-19

NA IBRAHIM ORUKO

AFISA katika afisi za chama cha ODM amepatikana na virusi vya corona Jumanne, katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna amesema.

Bw Ben Musungu ambaye ni mkurugezi wa masuala ya vijana amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi. Bw Sifuna alisema kwamba Bw Musungu anapokea matibabu na anaendelea vizuri.

“Tunawaomba wote waliotangamana na Bw Musungu kabla ya Juni 3 wajitokeze na kupimwa,” Bw Sifuna alisema alipohutubia wanahabari katika makao makuu ya chama hicho Nairobi.

Bw Musungu aligombea kiti cha ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kibra na akapoteza dhisi ya Imran Okoth.

Kulingana na Bw Sifuna, Bw Musungu alianza kuhisi joto jingi mwilini na maumivu mwilini wiki iliyopita. Alipelekwa katika hospitali kuu ya Aga Lhna eneo la Parklands ambapo mwanzo alipatikana akiugua nyumonia.

Hali iliendelea kuwa mbaya zaidi aliendelea kupimwa na kupatika na Covid-19. Bw Sifuna alisema kuwa hakuna uwekzekano kuwa kuna mfanyakazi mwingine katika ofisi ya ODM anayeugua virusi hivyo.

 

You can share this post!

Madiwani walivyopigana wakizozania kumng’oa Waiguru

SIHA NA LISHE: Ukitaka protini kula vyakula hivi

adminleo