Afisa wa polisi aliyetoweka mwaka mmoja uliopita bado hajapatikana

Afisa wa polisi aliyetoweka mwaka mmoja uliopita bado hajapatikana

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA wa polisi aliyetoweka zaidi ya mwaka mmoja uliopita hajapatikana bado, nduguye aliambia mahakama ya Milimani Nairobi Alhamisi

Afisa wa polisi wa utawala Bw John Arika anayehudumu katika kaunti ya Kisii alimweleza hakimu mwandamizi Bw Bernard Ochoi kwamba wamemtafuta ndugu yao Konstebo Abel Misati kila mahali bila mafanikio.

Bw Arika alisema kutoweka kwa ndugu yao kulizua wasiwasi mkubwa iwapo yu hai ama ameaga kwa vile mwili wake haujapatikana katika mochari yoyote katika kaunti za Machakos, Nairobi , Kiambu na kwengineko.

Bw Arika alisema kutoweka kwa nduguye kutoka kituo cha Polisi cha Kamkunji kuliguduliwa na mkewe Rachel alipomkosa kwa simu.Afisa huyo wa polisi alisema Abel hakuwa akipatikana katika makazi yake katika nyumba za polisi katika kituo cha Kamukunji.

Rachel alikuwa anaishi mashambani kaunti ya Kisii.Mwenzake Abel, Herman Muchiri , aliyezugumza na Arika alisema hawakuwa wameonana.Muchiri alidokeza alikuwa akishika doria zamu ya usiku naye Abel alikuwa zamu ya mchana.

Bw Arika alisema haya alipotoa ushahidi katika kesi ambapo raia wa Uganda Shariff Wanabwa na raia wa Kenya Phoebe Anindo wameshtakiwa kumteka nyara Abel Misati kwa lengo la kumuua.Wanabwa na Annido walishtakiwa pamoja na raia mwingine wa Uganda Martin Wasike aliyetoroka.

Polisi wanaendelea kumsaka nchini Uganda.Kufuatia kutoroka kwa Martin, maafisa watatu wa polisi wameshtakiwa kumsaidia kuchana mbuga.Shtaka la pili si dhidi ya Wanabwa na Anido ni kupatikana simu ya Abel Misati mnamo Aprili 7,2020 mtaani Eastleigh Nairobi.

Bw Arika alisema familia yao imemsaka ndugu yao kila mahali na wana matumaini huenda yuko hai kwa vile hawajawahi pata mwili wake.Dada yao maafisa hao wa polisi Bi Teresia Naftali alieleza mahakama alitumwa na nduguye (Arika) kumsaka Abel katika hospitali na mochari bila mafanikio.

Washtakiwa hao waliomba waachiliwe kwa dhamana lakini upande wa mashtaka ukapinga.Bw Ochoi aliwanyima dhamana na kuamuru waendelee kukaaa rumande hadi kesi ikamilike.Hakimu alimwagiza shahidi aliyesemekana hataki kutoa ushahidi afike kortini Septemba 10,2021 kesi itakapoendelea.

  • Tags

You can share this post!

Mjukuu wa Moi asalimu amri, sasa kupimwa DNA

Washirika wa vigogo wasisitiza mwaniaji wao ndiye astahili