Afisa wa uhasibu akana wizi wa Sh4.9M

Afisa wa uhasibu akana wizi wa Sh4.9M

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYAKAZI aliyehamisha Sh4.9m kutoka kwa akaunti ya mwajiri wake hadi kwa akaunti yake ameshtakiwa kwa wizi.

Martin Muriungi alikana aliiba Sh4, 955,045 kutoka kwa kampuni ya Direct Pay Limited. Alikuwa ameajiriwa kazi ya kuwahudumia wateja. Alidaiwa aliiba pesa hizo kati ya Feburuari 20 na Agost1 26, 2021 kutoka akaunti za kampuni hiyo zilizoko eneo la Kilimani, Nairobi.

Kampuni hiyo ufanya kazi ya uhasibu. Mahakama ilielezwa Muriungi alijihamishia mamilioni ya pesa kabla ya kujiuzulu. Hakimu mkazi Charles Mwaniki aliombwa na wakili Mukundi Gitau, Muriungi amwachilie mshtakiwa kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1milioni au pesa tasilimu Sh200, 000. Kesi itatajwa baada ya wiki mbili kutengewa siku ya kusikizwa.

You can share this post!

Wazazi wa mwaniaji Urais kufika Kortini kwa deni la Sh28.8M

ODM walalama Jubilee haipigii Raila debe

T L