Habari Mseto

Afisi ya Fedha Mandera yafungwa

October 27th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Afisi ya Fedha ya Kaunti ya Mandera imefungwa kwa muda kufuatia maafisa wa afisi hiyo kupatikana na virusi vya corona.

Bw Alinoor Mohamed Ali ambaye ni mhasibu na afisa mkuu wa fedha  aliandika ujumbe huku akisema kwamba afisi hizo zitabakia kufungwa kwa muda wa siku 14.

“Tumepta habari kwamba mmoja wenu amepatikana na virusi vya corona,” alisema. Afisi zetu zitabakia kufungwa ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona na kuruhusu kunyunyuziwa kwa  dawa.

Bw Ali alisema kwamba watu wachache ndio  watakaoruhusiwa kuingia afisi ambao wanashughulikia mambo ya maana.

Maafisa wote wa afisi ya fedha waliambiwa wote wajitenge kwa muda wa wiki mbili. Waliombwa pia watafute matibabu.