Habari Mseto

Afisi za afya Vihiga zafungwa

November 7th, 2020 1 min read

NA DERRICK LUVEGA

Afisi za afya za Kaunti ya Vihiga zimefungwa kwa siku 10 kwa taharuki kwamba kuna maafisa walioambukizwa virusi vya corona walipokuwa wakifanya kazi Kaunti ya Nakuru.

Mkurugenzi wa maswala ya afya Dkt Quido Ahindukha alisema kwamba waliamua kufunga afisi hizo ili waweze kunyunyuzia dawa afisi hizo.

Kufungwa kwa afisi hizo kulikuja siku chache baada ya kifo cha afisa wa afya aliyepatokana na virusi vya corona wiki iliyopita.

Dkt Ahindukha alisema kwamba maafisa wengine wa afya walikuwa wamefika kutoka mkutano Kaunti ya Nakuru.

Kaunti ya Nakuru inashuhudia mwogezeko wa maambukizi ya corona.

Maamuzi ya kufunga afisi hizo yalitangaziwa wafanyakazi kupitia notisi iliyotolewa na anyesimimamia shunguliza corona Dkt Kenneth Wafula.

Tafsri na Faustine Ngila