Habari Mseto

Afrika Kusini yarekodi visa vingi zaidi

June 28th, 2020 1 min read

 XINHUA na FAUSTINE NGILA
Afrika Kusini iliripoti visa 7,210 vya virusi vya corona, hii ikiwa idadi ya juu zaidi kuripotiwa tangu ugonjwa huo kuanza Machi.

Visa hivyo vimefikia 131,800, ilisema idara ya afya katika ripoti yake ya kila siku.

Nchi hiyo iliripoti vifo vingine  73 huku idadi ya vifo ikifikia 2,413.

Jimbo la Cape Magharibi linaongoza kwa maabukizi huku likiwa na visa 59,315, likifuatiwa na Gauteng likiwa na visa 34,285 na Cape Mashariki likiwa na visa 23,658.

Janga hilo hilo limeenea shuleni kufuatia kufunguliwa kwa shule Juni 8.

Zaidi ya wanafunzi 520 na walimu 1,169 walipatikana na virusi vya corona tangu shule zifunguliwe wiki tatu zilizopita idara ya masomo ikiongezea kwamba Cape Mashariki ina visa vingi huku ikirekodi visa 270.

Licha ya wito wa serikali wasifungue shule, waziri wa Elimu Angie Motshekga alisema kwamba wizara itaendelea na mipango yao ya kufungua shule.

Majimbo yaliyobaki bila kufungua shule yananamalizia mipango yao ya kufungua shule, waziri huyo alisema.