Afueni kambini Bandari FC ikikaribisha mabeki Odhiambo na Siraj kutoka mkekani

Afueni kambini Bandari FC ikikaribisha mabeki Odhiambo na Siraj kutoka mkekani

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

MABEKI mahiri wa Bandari FC, nahodha Bernard Odhiambo na Siraj Mohamed, wanatarajiwa kuwa kikosini kwa mchuano wa Ligi Kuu, dhidi ya FC Talanta mnamo Jumapili.

Mabeki hao wamekuwa mkekani wakiuguza majeraha. Odhiambo anatarajiwa kurudi uwanjani ikiwa kocha Andre Cassa Mbungo atampanga kwenye kikosi cha kucheza na Talanta ugani Mbaraki.Meneja wa Bandari FC, Albert Ogari, alisema Odhiambo ameshapona na amekuwa akifanya mazoezi magumu na wachezaji wenzake.

“Odhiambo amekosa mechi nyingi kutokana na jereha, lakini sasa yuko sawa. Ni uamuzi wa kocha kumtumia. Tunaamini mwanasoka huyu yuko tayari kuitumikia timu yake tena,” alisema.Mbali na Odhiambo, Ogari alisema kuwa Siraj aliyeumia wiki mbili zilizopita amepona kabisa.

“Ni furaha kuwa Siraj ameshapona kabisa na anatia zoezi na wenzake,” alisema.Kuhusu hali ya winga Shaaban Kenga, Ogari alisema kuwa mwanasoka huyo, ambaye alicheza mechi chache za msimu uliopita, ameanza mazoezi mepesi.

“Kenga anaendelea vizuri na mazoezi, lakini hajakuwa katika hali yake nzuri ya kuweza kucheza mechi. Nina imani kubwa baada ya siku chache zijazo za kufanya mazoezi na wenzake, ataweza kuingia uwanjani,” aliongeza.

Ogari aliwashukuru mashabiki waliofika uwanjani Mbaraki na kushangilia timu ya Bandari ikiliza AFC Leopards 1-0. Anatarajia wapenzi wa soka wa Pwani wataendelea kuiunga mkono Bandari itimize lengo lake la kutwaa ubingwa wa ligi

You can share this post!

Mvutano kuhusu RBK wachukua mkondo mpya

Ujenzi wa barabara waacha wakazi na kiu katika mitaa

T L