Afueni Rudisha akifanyiwa upasuaji na kutangaza atarejea kutimka hivi karibuni

Afueni Rudisha akifanyiwa upasuaji na kutangaza atarejea kutimka hivi karibuni

Na GEOFFREY ANENE OLUBUYI

MSHIKILIZI wa rekodi ya dunia mbio za mita 800 David Lekuta Rudisha anafurahia anaweza kurejea ulingoni hivi karibuni baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa skrubu kwenye mguu wake wa kushoto.

Bingwa huyo wa Afrika 2008 na 2010, Dunia 2011 na 2015 na Olimpiki 2012 na 2016 alitangaza hayo kupitia mtandao wake wa Twitter hapo jana. “Nafurahi kuwa Novemba 20 upasuaji wa mguu wangu wa kushoto kuondoa skrubu ulikuwa salama. Skrubu hizo zimekuwa mguuni mwangu kwa mwaka mmoja na nusu.

Sasa, nina matumaini kuwa nitarejea kukimbia hivi karibuni,” alisema mtimkaji huyo atakayesherehekea kufikisha umri wa miaka 33 hapo Desemba 17. Rekodi ya Rudisha kwenye mbio hizo za kuzunguka uwanja mara mbili ni dakika 1:40.91 ambayo imedumu tangu Agosti 9, 2012 alipotwaa taji lake la kwanza la Olimpiki jijini London, Uingereza.

You can share this post!

Kocha wa Sugar RFC hofu vifaa tegemeo kukosekana ufunguzi...

Mwendwa aponea ila hatarejea afisini FKF

T L