Habari za Kitaifa

Afueni wasahihishaji KCPE na KCSE 2023 wakipata malipo yao mapema

January 8th, 2024 1 min read

NA WANDERI KAMAU

KWA mara ya kwanza, serikali imetangaza kuwalipa wasahihishaji wa mitihani bila kuwacheleweshea pesa zao.

Mnamo Jumatatu, Waziri wa Elimu, Bw Ezekiel Machogu, alisema kuwa wasahihishaji hao watalipwa jumla ya Sh2.8 bilioni.

Wasahihishaji hao ni walimu walioshiriki kwenye zoezi la kusahihisha mitihani ya kitaifa ya Darasa la Nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE).

Katika miaka iliyopita, wasahihishaji hao wamekuwa wakilalamika kucheleweshewa malipo yao, hata baada ya kumaliza kusahihisha mitihani hiyo.

Serikali pia ilitangaza kutoa jumla ya Sh31.4 bilioni kufadhili elimu katika shule za msingi, Sekondari Msingi (JSS) na sekondari.

Shule za msingi zitapata Sh4.1 bilioni, JSS Sh7.6 bilioni huku shule za sekondari zikipokea Sh16.2 bilioni.