Dondoo

Afumaniwa akigawia ‘mjomba wa ughaibuni’ asali

May 5th, 2019 1 min read

Na TOBBIE WEKESA

UTAWALA, NAIROBI

ILIKUWA ni mguu niponye kwa kipusa mmoja eneo hili baada ya kunaswa na mume wake akigawa tunda.? Inasemekana kipusa alinaswa katika kitanda cha ndoa akiwa na jamaa mwingine wakilishana uroda.

Kulingana na mdokezi, jamaa alipenda kumtambulisha jamaa kwa watu kama kijana wa mjomba wake.

Mara kwa mara, jamaa huyo alikuwa akitembea na kipusa na yeyote akitaka kujua uhusiano kati yao, jibu lake kwao lilikuwa kwamba ni mmoja wa jamaa zake.

Duru zinasema kwamba mume wa kipusa alikuwa akishuku polo kwa sababu alikuwa akiwafahamu jamaa wote wa kipusa.

“Huyu ni mtoto wa mjomba wangu. Hauwezi kumjua kwa sababu hajalelewa wala kusomea humu nchini,” kipusa alimueleza mumewe.

Duru zinasema mume wa kipusa aliamua kuweka mtego. Inadaiwa aliamua kupanga safari ya ghafla huku akieleza mkewe ingechukua siku tatu.

Kulingana na mdokezi, polo alienda na kujificha katika hoteli moja iliyoko mtaani. Baada ya saa kadhaa alirudi kwake.

“Alipofika kwake, hakuamini macho yake. Alimkuta jamaa aliyeambiwa na mkewe alikuwa kijana wa mjomba akiwa juu ya mzinga akiguguna asali,” alieleza mdokezi.

Alipogundua kwamba mumewe alikuwa ameingia ghafla, kipusa aliruka na kumsukuma kisha akachomoka mbio lakini akamkamata.

“Unafikiri mimi ni mjinga. Nilijua mchezo wako siku moja utafika ukingoni,” polo alimkemea kipusa huku akimuangushia makofi. ? Kipusa alijaribu kuomba msamaha lakini wapi.

“Huwa nakupa kila kitu lakini bado unagawa nje. Mbona huridhiki,” polo alimkaripia kipusa. ? Wenyeji walibaki midomo wazi.

“Umenidanganya sana. Haya mambo hujaanza leo. Na kwanza mnafanyia vituko vyenu kwenye kitanda changu,” polo alimfokea.