Makala

AFYA: Jinsi ya kukabiliana na mafua, vidonda kooni na kikohozi

July 2nd, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Apple cider vinegar

ILI kupunguza maumivu yanayosababishwa na vidonda kooni, changanya kijiko kimoja cha Apple Cider Vinegar na maji moto.

Kunywa mchanganyiko huo ambao utasaidia kuua vijidudu vinavyosababisha uvimbe kooni.

Kitunguu saumu

Chukua vitunguu saumu kiasi, viponde halafu uvimumunye vikiwa vibichi kwa muda wa dakika 15.

Unaweza pia kuviponda, uvichanganye na asali, mafuta ya mizeituni au mboga za kienyeji ili kuifanya juisi yake ipate ladha kiasi.

Asali

Changanya asali kiasi unataka na maji moto, mafuta ya mizeituni au na dawa yoyote ya kiasili ambayo unajua fika inatumika kupunguza makali ya mafua. Kwa mara nyingi asali hujulikana kutibu vindonda kooni na pia kikohozi.

Maji ya chumvi

Mbinu hii ya kutibu vidonda hutumika na watu wengi nyumbani. Chemsha maji kikombe kimoja na uchanganye na kijiko kimoja cha chumvi kisha hakikisha yanatulia kooni kwa muda kiasi.

Juisi ya ndimu

Maji ya ndimu hukausha vidonda kooni na pia yanajulikana kwa kuzuia maradhi yoyote ya ugonjwa wa saratani. Unatakiwa kuchanganya ndimu na maji moto kisha uongeze asali au chumvi kabla kunywa.

Maji safi

Kunywa maji safi mengi husaidia kusafisha koo na kulizuia kukauka. Vilevile maji husaidia tumbo kwa sababu yana mchango muhimu katika usagaji wa vyakula tumboni.