Agizo vijana wanaoua wakongwe wanaswe

Agizo vijana wanaoua wakongwe wanaswe

Na HAMISI NGOWA

MRATIBU Mkuu wa serikali ya kitaifa katika ukanda wa Pwani, Bw John Elung’ata amewaagiza makamanda wa polisi katika kaunti na kaunti ndogo pamoja na machifu kuhakikisha vijana wanaojihusisha na mauaji ya wazee wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Akizungumza kwenye mpaka wa Kaunti za Kwale na Mombasa wakati wa hafla ya kuzindua Shule ya Upili ya Wasichana ya Mishi Mboko, Bw Elung’ata alisema mauaji dhidi ya wazee wanaotuhumiwa kwa uchawi na ushirikina yanaongezeka kwa kiwango cha kutisha.

Alisema ni jukumu la serikali kulinda mali na maisha ya wananchi na kuwahimiza maafisa wa usalama katika eneo hilo kuhakikisha kuwa wanaojaribu kuua wazee wanakabiliwa kisheria.

“Baadhi ya wazee sasa wanajaribu kupaka rangi nywele zao lakini vijana bado wanawafuata. Tafadhalini polisi na machifu, mkisikia mzee ameuawa kwa tuhuma za uchawi, msitafute mbali. Nendeni kwa vijana wa boma hilo na mtapata wauaji,” akaagiza.

Bw Elung’ata alisema anashangazwa na tabia ya baadhi ya vijana ya kuwahusisha wazee wakongwe na visa vya uchawi kila wanapokabiliwa na misukosuko au wanapokosa kufanikiwa maishani.

You can share this post!

Vyama vidogo vyadai kupuuzwa katika BBI

Jumla ya watu 563 wamekufa kutokana na virusi vya Corona

adminleo