Agizo wahudumu wa afya waondoke nyumba za serikali

Agizo wahudumu wa afya waondoke nyumba za serikali

Na LUCY MKANYIKA

Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta, imewaagiza wahudumu wote wa afya waliofutwa kazi kuhama nyumba za serikali mara moja ili zichukuliwe na wafanyakazi wapya wanaoendelea kuajiriwa.? ?

Gavana Granton Samboja alisema kwamba serikali yake itaendelea na mipango ya kujaza nafasi za wahudumu hao 400 wanaogoma ili kurejesha huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya vya umma.

Mapema mwezi jana, Bodi ya Huduma ya Umma ya Kaunti ilitangaza nafasi 317 za wauguzi na 92 za maafisa wa matibabu.

Akiongea akiwa Mwatate, Bw Samboja alisema kwamba tayari wahudumu 19 wameomba bodi warejeshwe kazini.

“Nimeomba Bodi ya Huduma ya Umma ya Kaunti kuwarudisha kazi wale walio tayari kurejea kazini. Lakini ninawahakikishia wakazi kwamba tutaawajiri wahudumu wapya wa afya hivi karibuni,” alisema.?Karani wa Kaunti, Liverson Mghendi, alisema kwamba wale wanaotaka kurudishwa kazini wamepatiwa fursa ya kuwasilisha maombi yao kwa bodi.

“Wahudumu wa afya waliofutwa kazi wanafaa kurudisha mali ya mwajiri na wale wanaoishi nyumba za kaunti wanafaa kuhama mara moja,” alisema.

Bw Mghendi alisema kwamba serikali ya kaunti imetatua matakwa mengi ya wahudumu hao licha ya uhaba wa pesa.

Alisema kwamba wahudumu 80 wamepandishwa cheo, 34 wamepatiwa majukumu mapya na 45 wamepatiwa gredi mpya.? Alisema kwamba bodi ya huduma ya kaunti inaendelea na mipango ya kuwapandisha vyeo wahudumu wengine 144.

Bw Mghendi alilaumu chama cha wauguzi nchini (Knun) na kile cha matabibu (KUCO) kwa kukataa kutii agizo la mahakama kwamba wakamilishe mfumo wa kutatua mizozo kati ya waajiri na wafanyakazi

You can share this post!

Biden aahidi kushirikiana na Afrika

Nitapigania kiti cha urais, sitateuliwa na Ikulu –...