Habari Mseto

Agosti 21 yatangazwa sikukuu ya Idd-ul-Azha

August 17th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

SERIKALI Ijumaa imetangaza Jumanne ijayo, Agosti 21 kuwa Sikukuu kwa Wakenya wote.

Katika taarifa rasmi iliyotumwa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Ijumaa, Waziri wa Masuala ya Ndani Dkt Fred Matiang’i alitangaza siku hiyo kama likizo kuadhimisha Idd-ul-Azha.

Wakenya wa dini zote kuungana na Waislamu kuadhimisha siku hii ambayo Ibrahimu alijitolea kumtoa mwanamwe kama sadaka kudhihirisha utiifu wake kwa Mungu.

Waislamu kwa sasa wamesafiri jijini Mecca, Saudi Arabia, kwa hajj, hafla inayotarajiwa kuendelea kati ya Jumapili na Ijumaa.

“Umma unafahamishwa kwamba siku ya Jumanne, Agosti 21, 2018 itakuwa Sikukuu kuadhimisha Idd-ul-Azha, 2018,” alisema Dkt Matiang’i katika tangazo hilo.