Habari Mseto

Aibu baba kumbaka bintiye

August 2nd, 2020 1 min read

STEPHEN ODUOR na FAUSTINE NGILA

Msichana wa miaka sita anapigania uhai wake kwenye hospitali ya rufaa ya Hola baada ya kubakwa na babake mzazi.

Msichana huyo aliletwa hospitalini na wazazi wake waliosema kwamba aliumia akicheza na mti ila uchunguzi ulionyesha kwamba wazazi walidanganya ili wamwokoe babake kutokana na aibu.

Afisa mkuu wa maswala ya uzazi Abdiga aliambia Taifa Leo kwamba msichana huyo akilazwa hapo hospitalini alikuwa amepasuka sana sehemu nyeti na kupoteza damu nyingi.

“Aliletwa akiwa kwenye hali mbaya na alikuwa na amepoteza damu mingi na maumivu mingi.Kwa hivo tulifanya tuwezavyo kufanya uuchunguzi kibinafsi ,” alisema.

Kulingana na kamanda wa polisi wa Hola Peter Ekuthi msichana huyo salifichua kwamba banbake alimpa Sh 100 ili ashikilie kuwa aliumizwa na mti akicheza,na kumtishia kumuua akisema kilichojiri,”aliongeza.

Mwanaume huyo anayejuilikana kama Gavana mwenye miaka 40 amekamatwa tayari na atafikishwa kortini.