Habari Mseto

Airtel sasa yalenga kuingia NSE kushindana na Safaricom

August 21st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

SAFARICOM itakabiliwa na wakati mgumu sokoni ikiwa Airtel itaorodhesha hisa zake katika soko la hisa jijini Nairobi (NSE).

Airtel imedokeza mpango huo ambao unatarajiwa kuibua ushindani mkubwa katika soko la mawasiliano.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Kenya Prasanta Das Sarma, suala hilo linajadiliwa kwa kiwango cha washikadau.

Ikiwa itaorodheshwa, Airtel Kenya itakuwa kampuni ya pili ya mawasiliano ya simu kuorodheshwa NSE baada ya Safaricom.

Safaricom wiki jana ilitangazwa kuwa ya thamani ya Sh1.15 trilioni katika NSE.