Habari

Aisha Jumwa aachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni

October 17th, 2019 1 min read

Na MISHI GONGO

MAHAKAMA ya Mombasa imemuachilia mbunge wa eneobunge la Malindi, Aisha Jumwa kwa dhamana ya Sh1 milioni.

Hakimu mkuu mkazi Vincent Okello ametupilia mbali ombi la upande wa mashtaka kutaka kumziuilia mbunge huyo kwa siku 21 akisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuendelea kumzuilia.

Hakimu huyo aliwataka maafisa wa polisi kuwa na ushahidi wa kutosha kabla ya kumkamata mshukiwa.

Jumwa alikamatwa Jumanne usiku baada ya vurugu zilizotokea nyumbani kwa mgombea wa ODM wa kiti cha udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa Ganda.

Mgombea wa ODM ni Reuben Katana.

Wakati wa vurugu hizo, mwanamume alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi.