Habari Mseto

Aishtaki serikali kwa kufunga shule

August 26th, 2020 1 min read

NA Joseph Wangui
Mzazi wa Kaunti ya Nairobi ameishtaki serikali kuu kwa kuendelea kufunga shule kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Joseph Enock Aura alisema kwamba kufungwa kwa shule ni ukukaji wa haki za wanafunzi.

Rais Uhuru Kenyatta aliamuru kufungwa kwa shule mapema mwaka huu Mechi 13  baada ya Kenya kuripoti kisa cha kwanza cha corona.

Shule zilikuwa zifunguliwe Septemba lakini kwasababu ya kuongezeka kwa virusi vya corona Profesa Magoha alisema kwamba shule zitaendelea kufungwa mpaka Januari 2021.

Kufikia Agosti 24, Kenya imerekodi visa 32,557, vikiwemo vifo 554 na watu 18,895 kupona.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA