Dondoo

Ajabu mke akiambiwa apeleke mali ya mpango wa kando na huko

March 18th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

KALAMENI mmoja wa hapa alimlazimisha mkewe kurudisha alikotoa bidhaa alizofika nazo nyumbani akishuku ni mpango wa kando wa mwanadada huyo aliyezinunua.

Mwanadada huyo alikuwa na tabia ya kuchelewa kufika nyumbani, jambo ambalo lilimtia wasiwasi mumewe.

Siku ya tukio, demu alifika nyumbani na shopping ya nguvu sana baada ya kuangukia marupurupu kazini.

Mumewe alichemka kwa hasira na kumtaka arudishe bidhaa hizo alikozitoa na kuapa kwamba kama hangerudisha angemtaliki.

“Za mwizi ni arobaini, ulidhani utachepuka hadi lini kwa siri? Kama unafikiri utaweza kulisha familia yangu kwa mali ya mpango wa kando sahau,” jamaa alifoka hasira.

Mkewe alicheka na kumweleza alikotoa pesa.