Habari Mseto

Ajabu ya mteja kuwa na mawakili 32

August 30th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

NAIBU wa Jaji Mkuu DCJ Philomena Mwilu anatetewa na mawakili 32 katika kesi inayomkabili ya ufisadi.

Akiwataja mmoja baada ya mwingine, wakili James Orengo anayewaongoza alimweleza hakimu mkuu Bw Lawrence Mugambi kuwa kila mmoja wao atashiriki katika kesi hiyo.

“Idadi hii kubwa ya mawakili wanaomtetea Jaji Mwilu ni ishara kwamba anaonewa na wanataka kushiriki kuibomoa kabisa kesi hii aliyoshtakiwa,” alisema Bw Orengo

Bw Orengo alisema kuwa mashtaka dhidi ya Jaji Mwilu hayana mashiko kisheria na yamewassilishwa dhidi yake kumfedhehesha tu.

Mawakili hao watafanya utafiti wa kina kuidungua kesi hiyo inayoongozwa na naibu wa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Bi Dorcus Oduor.